SHULE ndio kila kitu katika maisha yanayoendelea kwa sasa maneno hayo
anayasema mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu Swahiliwood Julieth
Samson kakuru ‘Kemmy’ msanii huyo mtunzi na mwigizaji wa filamu Bongo
amesema kuwa vijana hawataki kusoma kwanza ndio waje katika uigizaji
jambo linalofanya filamu zetu kukosa hadithi na uhusika unaotakiwa
katika filamu husika.
Kemmy akiwa katika pozi la picha.
“Ninawapenda
sana waigizaji chipukizi wanaoamua kuingia katika tasnia ya uigizaji
lakini kabla ya kukimbilia huku wakiitafute elimu kwanza isije
ikawaacha, kulingana na hali ya mabadiliko ya nchi kusoma ni lazima si
jambo la hiari tena, mtu ukielimika uwezo wa kufikiria unakuwa juu, na
kazi yako itakuwa bora,”anasema Kemmy.
Kemmy anaangalia filamu nyingi haoni kitu kipya zaidi ya kurudia
majina hata wakati akiandika filamu yake ya Nguvu ya Imani (Power of
Faith) anasema kuwa alikuwa na wakati mgumu kwani alikuwa akifikiria
jinsi gani kazi yake ingepokelewaje, lakini Filamu ya Nguvu ya Imani
inauzika sana kutoka na ujumbe uliopo ndani ya filamu hiyo ikiongelea
uponyaji wa ndoa zilizovurugwa.
No comments:
Post a Comment