TIMU ya mastaa waliokuwa wakishabikia timu ya Bongo Movie wamemzodoa mwigizaji mwenzao, Flora Mvungi baada ya kumuona anashabikia Timu ya Bongo Fleva anayochezea mumewe, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’.
Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Taifa,
jijini Dar ambapo mastaa hao waliibua minong’ono mara baada ya kuona
Flora anashangilia pindi timu ya Bongo Fleva inashambulia lango la Bongo
Movie.
“Mh! Tumekaa naye tukijua ni mwenzetu kumbe hamna lolote, bora tumtenge asituharibie shughuli,” alisema staa mkubwa wa kike aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini.
Baadhi ya mastaa ambao walikuwa wamekaa pamoja katika jukwaa na Flora ni pamoja na Shamsa Ford, Rechael Haule ‘Recho’, Chuchu Hans na wengineo.

Credit: GLP
No comments:
Post a Comment