Baada ya kuzagaa kwa habari zikimtumu
mwanadada wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka aka Odama kwamba huzifanyia
makeke yaphotoshop picha zake na kuwadanganya wananchi kuwa amezipigia
Ulaya, ameongea na na mwandishi wetu kukanusha huku akionesha picha
halisi zinazomuonesha akiwa mbele.
Baada ya tuhuma hizo kumkabili Odama,
Mwandishi wetu alimtafuta mwanadada huyo wa filamu na ndipo
alipokanusha tuhuma hizo na kusema hakufanya kitu kama hicho na kwamba
waliosema hivyo wanania mbaya naye.
Ili kukata ‘ngebe’ za manisnitch hao Odama ametutumia picha hizi za ushahidi kwamba alikuwa nje ya nchi kama alivyosema.
“Kuna watu wanakosa vya kufanya ndio
maana wanakaa na kuanza kuzusha vitu ambavyo hawana uhakika navyo so
siwashangai kwakuwa binadamu tunatofautiana upeo,”Odama
CHANZO NI 2JIACHIE
No comments:
Post a Comment