EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 19, 2013

Nyerere: JK ataje wauza ‘unga’.

KUCHAFUKA kwa Tanzania kimataifa ikituhumiwa kuwa ‘lango’ la kusafirisha dawa za kulevya kumewalazimisha wanasiasa kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwakamata haraka vigogo wanaohusika na biashara hiyo.

Mmoja wa wanasiasa hao, Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amelazimika jana kutoa taarifa kwa vyombo vya habari nchini akimwomba Rais Kikwete kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika ambao aliwahi kudai anawajua kwa majina.

Nyerere ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, katika taarifa yake alisema Rais Kikwete ndiye aliyeutangazia umma kuwajua wahusika wa biashara hiyo, lakini ameshindwa kuwataja, badala yake kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaojihusisha na biashara hiyo kiasi cha kuchafua jina la nchi katika ngazi za kimataifa.

Alisema kushamiri kwa biashara hiyo haramu kiasi cha kuilazimu serikali kutangaza kuwa janga la taifa kunatoa picha kwamba imezidiwa nguvu na vigogo wanaoendesha biashara hiyo.

“Rais Kikwete alisema anawafahamu wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na alipiga hatua kubwa zaidi na kusema wamo pia viongozi wa dini, lakini nashangaa kuona sasa hajafanya hivyo, licha ya maaskofu kumtaka awataje hadharani,” alisema Nyerere.

Mbunge huyo alisema ukimya wa rais, huku hali ikizidi kuwa mbaya kutokana na kuwapo kwa madai ya kukamatwa kwa wasichana wawili Watanzania nchini Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya yenye thamani ya sh bilioni sita, kunazidi kuzua maswali mengi.

“Ukimya wa rais unaweza kuchukuliwa kuwa serikali yake haina tena ubavu wa kupambana na wauza unga, jambo ambalo ni hatari kwa vijana wetu,” alisema.

Mbali na kutaka rais kuchukua hatua, Nyerere pia aliwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuwaeleza Watanzania kulikoni hadi Tanzania inakuwa uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Mbunge huyo alimtaka pia Kamishina wa Tume ya Dawa za Kulevya kujieleza, iweje kiasi kikubwa cha dawa za kulevya katika tukio la hivi karibuni la kukamatwa kwa wasichana hao nje ya nchi kiliweza kupitishwa katika uwanja wa ndege bila kujulikana.

Watu wengine maarufu waliowahi kuzungumzia hatari ya biashara hiyo na tuhuma za kuhusisha watu wazito nchini ni pamoja na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (CCM).

Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya ilibainisha kuwa kati ya mwaka 2008 na 2012, watuhumiwa 10,799 walikamatwa na dawa za kulevya hapa nchini, wengine 240 wakikamatwa na dawa hizo katika nchi za Brazil, Pakistan, China na Afrika Kusini, jambo ambalo limetia dosari kubwa katika jumuiya ya kimataifa.
Via Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate