Mwanafunzi wa darasa la tatu katika
shule ya msingi Kizega wilayani Iramba Bi. Mariamu Alphonce mwenye umri
wa miaka kumi ameuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na kucharangwa kwa
panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kaka yake bwana Elibariki
Alphonce.
Akieleza kwa uchungu baba wa mtoto huyo bwana Alphonce Msengi
amesema alipofika nyumbani kwake majira ya saa kumi na moja jioni
alikuta damu nyingi na alipo angali vizuri alimuona mtoto wake Mariamu
Alphonce akiwa amekatwakatwa kwa mapanga na tayari alikuwa ameshafariki.
Bwana Msengi baada ya kuona hivyo alipiga yowe na walikuja
majirani na watoto na wakamwambia tumemuona mtoto wako Elibariki akiwa
na mapanga mawili akikimbia huku akiwa hana nguo.
Wakieleza mwenyekiti
wa kitongoji Bi Vailet Mbigu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizega
bwana Elisante Gyuzi wamesema pamoja na shule kuandaa taratibu zote za
mashishi , kijana aliyefanya unyana huo huwa anavuta bangi na mara
nyingi alikuwa akisikika kumtishia kumuuwa baba yake kwa kumkata kwa
panga.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya
Iramba daktari Timoth Sumbe amesema wamempokea Mariamu Alphonce akiwa
ameshafariki huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwakatwa sehemu
ya shingoni,kichwani.
Akiongea kwa simu kamanda wa jeshi lapolisi mkoani Singida bwana
Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na jeshi lake
lina endelea kumsaka mtuhumiwa bwana Elibariki Alphonce ambaye
alitoweka baada ya mauaji ili aweze kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment