Msanii mkongwe wa kizazi kipya Joseph Haule a.k.a Profesa Jay amempoteza
mama yake mzazi jana baada ya kugongwa na gari alipokuwa akienda
kununua mahitaji muhimu ya nyumbani.
Akiongea na Times fm Fred Mariki maarufu kama Mkoloni kutokea msibani
amesema mama Jay baada ya kugongwa na gari alimpigia simu mwanae
kumwambia amepata ajali jambo lilimpa matumaini msanii huyo kwa kufikiri
huenda hali ya mama yake haikuwa mbaya sana. Walipompeleka hospitali ya
Tumbi Kibaha ndio ikathibitishwa ameshafariki dunia.
Msiba uko Mbezi mwisho nyumbani kwa Profesa J na mipango ya mazishi inaendelea.Mamu Africa blog inatoa pole kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
Msiba uko Mbezi mwisho nyumbani kwa Profesa J na mipango ya mazishi inaendelea.Mamu Africa blog inatoa pole kwa msiba huo na Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.
No comments:
Post a Comment