Mghani
mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa
msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima
la ujasiliamali mapema siku ya jana kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika
ukumbi wa Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora
mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa
na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Baadhi
ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa
vijana ililiyofanyika siku ya jana kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya
mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba
Levo,Amin,Stamina na wengineo.
Mkuu
wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu
akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo
mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na
kutokata tamaa,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kutoka
tamaa kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake waitumie vizuri
katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa
alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki
wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa
NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Mwakilishi
wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan
akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama
amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote atakayejiunga na
shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo
na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
Baadhi
ya Wakazi wa Tabora wakifuatilia kwa makini semina ya ujasiliamali
iliyokuwa ikiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya
mkoa wa Tabora mapemasiku ya jana.
Picha ya pamoja,kiukumbusho zaidi,Msanii Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Diamond,akiwaimbisha washiriki wa
semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye ukumbi wa
Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora,kushoto kwake
ni Bwa.Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. .
Mmoja
wa akina Mama wajasiliamali kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria akiwa
na bidhaa zake alizozitengeneza yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza
ndani ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo imewahusisha wadau
mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi mbalimbali
wa mji wa Tabora,Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
Pichani
kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media
Group,Ruge Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga ( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tabora),Mh. Elibariki Kingu wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa
na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi
Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge
Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya
ukumbi kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa
Tabora.
Sehemu
ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim
Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa
Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya
Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben
Temu kutoka kampuni ya Lake Oil
Baadhi ya Wasanii mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.
Baadhi
ya wakazi wa Tabora wakiwa kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi
Student's Center mkoani Tabora mapema siku ya jana,ambapo mada mbalimbali
zimezungumzwa,ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,mikopo,akiba
sambamba na namna ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.
No comments:
Post a Comment