Dar es Salaam.
Kampuni ya Simu za Mikononi Vodacom kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imezindua mfumo wa ulipaji ada za magari kupitia huduma ya M-Pesa.
Kampuni ya Simu za Mikononi Vodacom kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imezindua mfumo wa ulipaji ada za magari kupitia huduma ya M-Pesa.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom,Kelvin Twissa alisema jana kuwa ulipaji huo utawaepusha Watanzania kukumbana na foleni zisizo za lazima wakati wa ulipaji wa ada za magari.
“Ni wakati mwingine M-pesa inawapa walipakodi na wananchi utaratibu mwepesi na salama, huku wakiwa na uhakika wa kulipa ada za leseni ya magari kwa urahisi wakati wowote” alisema
Alisema Vodacom itaendelea kuuwezesha mfumo wa M-pesa kuwa wenye kutoa suluhisho la masuala mengi ili kukidhi matarajio ya kampuni hiyo ya kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa mamlaka ya mapato katika ukusanyaji wa ada za magari.
Alisema TRA ina imani kuwa ushirikiano wake na
Vodacom utakuwa wenye tija zaidi katika siku zijazo kwa kuhakikisha
mfumo wa M-pesa unatoa uwezo kwa walipakodi.
Aliongeza kuwa inakadiriwa kuwa kwa kipindi cha
wiki mbili TRA imekusanya kiasi cha Sh2 bilioni ikiwa ni makusanyo
kutoka M-pesa
No comments:
Post a Comment