Rose Muhando, Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja, Upendo
Nkone, Edson Mwasabwite, Jennifer Mgendi, Christina Matai, na wengineo
wengi tu watakuwepo kumsindikiza Bahati Bukuku wakati wa tamasha la
kuzindua DVD ya dunia haina huruma bure kabisa.
Katika mahojiano na Silas Mbise kupitia Gospel Celebration ya WAPO Radio FM, Bahati anaeleza sababu ya kufanya uzinduzi huo bure ni kwamba anahitaji watu wengi wafike kwenye ukumbi wa PTA kwenye viwanja vya sabasaba.
Kwa kuwa imekuwa desturi ya baadhi ya watu kutofika kutokana na kukosa hela ya kiingilio, sasa hapa anawaambia kuwa wajipange kwa nauli yao tu na kwenda siku hiyo (Jumapili tarehe 8) wapate kununua DVD yake kwa mara ya kwanza itakapoanza kuuzwa.
Kwa maelezo ya Bahati Bukuku, basi hauna sababu ya kukosa kuhudhuria
kwenye tamasha hilo litakaloanza mishale ya saa 8 mchana na kuendelea.
KIINGILIO NI BURE LEO HIIIIIII TPA SABASABA
KIINGILIO NI BURE LEO HIIIIIII TPA SABASABA
No comments:
Post a Comment