TANZANIA,
Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Gambia usiku kwenye Uwanja wa
Independence mjini Banjul katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kuhitimisha
hatua ya awali ya kuwania Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini
Brazil.
|
Mbaya wetu; Mustafa Jaju amefunga mabao yote ya Gambia |
Kwa
matokeo hayo, Stars imemaliza na pointi sita katika nafasi ya tatu,
nyuma ya Morocco wa pili na Ivory Coast vinara wa kundi, wakati Gambia
wameshika mkia kwa pointi zao nne, huu wa leo ukiwa ushindi wao pekee
kwenye kundi hilo.
|
Stars imechapwa 2-0 Gambia |
Mbaya
wa Stars leo alikuwa ni mshambuliaji Mustapha Alasan Jarju mwenye umri
wa miaka 27 aliyefunga katika dakika ya 45 na 51 mabao yote hayo.
Mchezo
mwingine wa kundi hilo kati ya Morocco na Tembo wa Ivory Coast
unaendelea kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, Simba
wa Atlasi wakiwa wanaongoza 1-0 dakika za lala salama, lililofungwa na
Youssef El-Arabi dakika ya 53.
|
Amechemsha; Stars imeshindwa kupata mafanikio chini ya Kim Poulsen |
Matokeo
haya yanaamisha kufeli vibaya kocha Mdenmark, Kim Pouslen baada ya
awali Tanzania kukosa tiketi za kucheza Fainali za AFCON na CHAN chini
yake.
Kim
alirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen Mei mwaka jana
na leo ulikuwa mchezo wake wa 16 kazini, akifungwa saba, sare nne na
kushinda mitano.
Kikosi
cha Gambia kilikuwa; B. Sanyang, A. Mansally, O. Colley, S. Marreh, T.
Jaiteh, E. Sohna, H. Barry, S. Faal, M. Jarju na M. Ceesay.
Stars;
Juma Kaseja, Erasto Nyoni/David Luhende dk 70, Vincent Barnabas, Mrisho
Ngassa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Amri Kiemba, Khamis Mcha ‘Vialli’/Jum
a Luizio dk 61, Haroun Chanongo, Frank Domayo na Simon Msuva.
Credit to BIN ZUBERY BLOG
No comments:
Post a Comment