DEREVA wa Shirika la Kimataifa linalo hudumia wakimbizi (UNHCR)
katika Mkoa wa Katavi, Amani Malilo, amehukumiwa kifungo cha miezi
sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kuishi na msichana mwenye
umri wa miaka 16.
Msichana huyo ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya
Sekondari ya Mishamo, wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Wilaya, Chiganga Ntengwa, baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa
mashitaka.
Awali katika kesi hiyo, Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa
Polisi, Razalo Masembo, aliileza mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa
hilo Novemba 27 na Desemba 25, mwaka jana.
Ilidaiwa kuwa baada ya kumtorosha msichana huyo alisafiri naye hadi
wilayani Kasulu, mkoani Kigoma na baada ya kutoka Kasulu alimhifadhi
nyumbani kwake na kumuachia sh 5,000 kila siku kwa ajili ya chakula.
Mshitakiwa inadaiwa waliendelea kuishi na kulala pamoja na msichana
huyo kwa kipindi chote hicho wazazi wa binti huyo wakiwa wanaendelea
kumtafuta hadi Machi 6, mwaka huu.
Inaelezwa kuwa siku hiyo, mtuhumiwa alisahau simu ndipo msichana huyo
alipoichukua na kuitumia kumpigia mama yake kumjulisha mahala alipo.
“Baada ya wazazi kufikishiwa taarifa hizo walilazimika kwenda Kituo
cha Polisi cha Mpanda mjini na siku hiyo hiyo ya tarehe 26 Machi
mwaka huu mnamo majira ya saa tisa usiku polisi walifika nyumbani kwa
mshitakiwa katika Mtaa wa Mji Mwema mjini hapa na kumkuta mwanafunzi
huyo akiwa ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi na mshitakiwa Amani,”
alisema.
No comments:
Post a Comment