Zanzibar.
Taasisi za kiraia Zanzibar zimesema hazijawahi kushirikishwa katika kuiboresha Muswada wa sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya Tanzania.
Taasisi za kiraia Zanzibar zimesema hazijawahi kushirikishwa katika kuiboresha Muswada wa sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya Tanzania.
Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal(kulia), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki mara baada ya kufungua Kongamano la Katiba Mpya na Nafasi ya Wazenjibara (Wazanzibari wanaoishi bara) jana.
Taasisi hizo saba ambazo zinaongozwa na Baraza la Katiba Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Pr. Abdul Sharif zilisema Bunge halijawatendea haki kwa kunyimwa fursa ya kutoa maoni katika sheria hiyo. Waliyasema hayo huko Bwawani Zanzibar walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jana.
Katibu wa Zanzibar Youth Forum Alimasi Mohammed Ali alisema kushirikishwa Serikali ya Mapinduzi haina maana kwamba na wananchi wameshirikishwa.
“Muswada ule ulipokuja mwanzo, viongozi wa serikali waliitwa Bwawani na sisi raia wa kawaida tuliitwa katika skuli ya Haile Salasi kutoa maoni yetu” alisema Ali.
Alisema haoni sababu kwa muswada huu wa sheria hiyo kupewa fursa serikali peke yake na wao kama raia wakaonekana kama hawana maana.
“Walijua fika kwamba Wazanzibar hawawezi kukubali kuwa wachache katika Bunge la Katiba na bara kuwa wengi” alisema Ali.
Alifananisha na tume ya mabadiliko ya katiba kwamba ilikwenda kwa wananchi mara mbili tofauti. Kwa nini kamati ya Katiba na Sheria ishindwe. “Hatukubaliani hata siku moja kwa
Bara wawe na 64% na Zanzibar kubakia na 36% wakati ni nchi mbili sawa katika Muungano” alieleza Ali.
Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar Pr Abdul Sharif alisema kwa mujibu wa sheria ingalikuwa vyema Muswada huo ukaonekana katika magazeti ili wananchi watoe maoni yao.
“Mimi mwenyewe nilikuwa na mapendekezo yangu lakini hawakunipatia fursa ya kutoa mawazo yangu” alisema Pr. Sharif.
Alisema wameutoa mswada huo katika kabati na kuupeleka Bungeni tu, halafu wanajidai wananchi wamepata fursa si kweli. Aliendeleaa.
Taasisi ambazo zimeshiriki mkutano huo ni pamoja na TAMWA, Zanzibar Youth Forum, Zanzibar Law Society, Baraza la Katiba, Pemba Press Club, Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar na ZAFELA.
No comments:
Post a Comment