KIPA namba moja wa Simba, Abel
Dhaira amelazimika kuiacha klabu yake na kurudi kwao Uganda, baada ya
kuitwa haraka na mahakama ya nchini humo.
Hatua hiyo inakuja
kufuatia Dhaira ambaye kwa sasa ndiye kipa muhimu katika kikosi hicho,
kutoonekana katika mazoezi ya siku mbili ya kikosi hicho, huku kukiwa na
taarifa zinazokinzana kuwa kipa huyo anaumwa.
Mmoja wa viongozi
wazito wa Simba ameliambia Championi Ijumaa kuwa, kipa huyo amelazimika
kurudi Uganda kufuatia kukabiliwa na kesi inayomhusisha kununua kiwanja
ambacho tayari kilishauzwa kwa mtu mwingine.
Bosi huyo, ambaye
aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema Dhaira alishaomba ruhusa
hiyo muda mrefu lakini msisitizo juu ya hilo ulikuja kumtaka kipa huyo
kuwasili haraka kushughulikia kesi hiyo ya kiwanja kilichopo katika Mji
wa Jinja nchini Uganda.
“Alikuwa akiomba ruhusa muda mrefu, naona
sasa atakuwa ameshakwenda huko kutokana na kuitwa haraka kufuatilia kesi
hiyo, kesi yenyewe imetokana na Dhaira kununua kiwanja eneo la Jinja
lakini baada ya kununua akapata taarifa kuwa kiwanja hicho tayari
kilishauzwa kwa mtu mwingine, wakashindwa kuelewana na ikafunguliwa
kesi, sasa ndiyo amekwenda huko,” alisema bosi huyo.
CREDIT GLP
No comments:
Post a Comment