Baadhi ya majaji wakijadiliana jambo, Nisha (kushoto), Wastara (katikati) na Benny Kinyaiya (kulia).
MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ jana aliendesha zoezi
la kuwafanyia usahili wasanii chipukizi ambapo alikuwa akitafuta
wasanii 50 kwa ajili ya kufanya nao kazi katika kampuni yake ya Nisha’s
Film Production.
Zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa Vijana,
Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo majaji waliokuwa wakiwafanyia
usahili wasanii hao ni, Wastara Juma, Idrisa Makupa ‘Kupa’ Jimmy Mafufu,
Benny Kinyaiya na Nisha mwenyewe.
(Habari / Picha: Na Gladness Mallya / GPL)
No comments:
Post a Comment