Van Persie akielekwzwa jambo na David Moyes |
Robin
van Persie amekanusha madai kwamba hana furaha kufanya kazi chini ya meneja
mpya wa Manchester United, David Moyes.
Mshindi
huyo wa kiatu cha dhahabu misimu miwili mfululizo iliyopita, Robin van Persie alipata
ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa chini ya Sir Alex Ferguson
aliyekuwa akitumikia msimu wake wa mwisho Old Trafford.
Mdachi
huyo ameanza vema pia msimu huu, alifanikiwa kuzamisha mipira miwili wavuni
Manchester United iliposhinda Ngao ya Jamii dhidi ya Wigan na magoli mengine
mawili kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Swansea.
Van
Persie tangia hapo hajafunga tena. Hakufanikiwa kupata nafasi ya kufanya
chochote pale walipotoa sare dhidi ya Chelsea na mechi ya Jumapili iliyopita
dhidi ya Liverpool walipotoka Anfield mikono ikiwa chini kwa kichapo cha bao
1-0.
Lakini
mdachi huyo mwenye umri wa miaka 30 amesisitiza kuwa habari hizo si za kweli
kabisa, amekaririwa akisema: “Ni jambo kubwa kwangu kufanya kazi na meneja mpya
David Moyes. Ana aina na mbinu mbalimbali za ufundishaji, nazipenda.
“Namfurahia
Moyes. Anafundisha, yuko karibu na wachezaji na wafanyakazi wengine pia,
anatuandaa vema kwa mechi inayofuata. Na hilo linatuleta pamoja.
“Kwa
bahati njema, ushindi wa ubingwa msimu uliopita umetupa njaa ya kutaka tena.”
Robin
van Persie alikuwa lulu kwa Manchester United mwaka jana kipindi cha usajili,
lakini David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson ameshindwa kuleta
mchezaji nyota Old Trafford.
Hatimaye
United imefanikiwa kumyakua mchezaji wa kimataifa raia wa Ubelgiji Marouane
Fellaini kutoka Everton dakika za majeruhi kabla ya dirisha la usajili
kufungwa. Lakini vilevile waliwakosa wachezaji wengine waliokuwa kwenye rada
yao wakiwamo, Cesc Fabregas, Leighton Baines, Ander Herrera, Cesc Fabregas,
Sami Khedira na Fabio Coentrao.
Manchester United walikuwa na shauku ya kumleta Marouane Fellaini kabla ya dirisha la usajili kufungwa, na walifanikiwa kumnasa kwa kitita cha paundi milioni 27.5.
No comments:
Post a Comment