Ligi
Kuu ya
Vodacom itaendelea katika viwanja saba nchini huku mabingwa
watetezi timu ya Young Africans ikishuka dimbani kucheza na wenyeji
Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.
Young Africans imefanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika uwanja wa
Sokoine ikiwa na wachezaji wake wote wakiwa katika hali nzuri kiafya,
morali na ari ya juu kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Mara
baada ya mazoezi hayo kocha mkuu Ernie Brandts amesema kikosi chake
kipo katika hali nzuri na hakuna mchezaji hata mmoja majeruhi kuelekea
kwenye mchezo huo ulioteka hisia nyingi za wakazi wa mkoa wa Mbeya.
Watoto
wa jangwani watashuka dimbani kuhakikisha wanapata pointi 3 katika
mchezo huo ili kujiweka katika mazunguri mazuri ya kukaa kileleni mwa
msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.
Young Africans inashia
nafasi ya pili katika msimamo baada ya kufikisha pointi 4 na mabao sita
ya kufunga na mabao mawili ya kufungwa kufuatia ushindi wa mabao 5-1
dhidi ya wauza mitumba wa Ilala Ashanti United na kutoka sare ya bao 1-1
dhidi ya Coastal Union.
Kiingilio cha mchezo huo kitakua ni TSHS 5,000/=
Mchezo
utaanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na tiketi
zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika vituo vifuatavyo:
1.Mwanjelwa Sokoni, 2.Kabwe, 3.Mbalizi, 4.Stand Kuu, 5.Uyole, 6.Stopa Enterprises, 7.Holiday, 8.Iyunga, 9.Uhindini, 10.Sokoine
No comments:
Post a Comment