EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, November 28, 2012

MAMA WA RAY C AFUNGUKUKA MWANAE KUZUSHIWA KIFO.

MAMA mzazi wa Ray C amefunguka kuhusu uvumi ulizogaa kuwa mwanae amefariki dunia.

Mapema usiku huu, zilisambaa habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwimbaji nyota wa kike Ray C amefariki dunia.
Akiongea kwa njia ya simu kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM muda mfupi uliopita, Mama wa Ray C alisema uvumi huo si wa kweli na hajui habari hizo zimetokea wapi.
“Nakataa kabisa, tena nakataa kwa jina la Yesu, hizo habari ni za uongo, alisema Mama huyo na kusema mwanae anaendelea vizuri na matibabu, anakula vizuri na anapata usingizi.Via Saluti 5

Tuesday, November 27, 2012

SAFARI YA MWISHO YA JOHN STEPHANO MAGANGA, ANGALIA PICHA HIZI KISHA UTAJAZA MWENYEWE NANI ALIKUWA MSIBANI NANI ALIKUWA KIJIWENI.

Habari na Saluti 5-Tanzania www.saluti5.com
HIZI ni picha 16 miongoni mwa picha nyingi zinazoonyesha jinsi mazishi ya John Stephano Maganga yalivyofanyika leo mchana kwenye makaburi ya Kinonndoni.
Katika picha hizi utashuhudia matukio tofauti na namna watu walivyosindikiza John Maganga, wengine wakionekana kweli msiba umewafika, wengine kama wako kijiweni na wengine kama wako kwenye sherehe fulani. Zitazame kwa makini labda na wewe utagundua kitu fulani.
                             CHANZO CHA HABARI NA SALUTI 5 www.saluti5.com

NAPE AWAKILISHA CCM KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MSANII WA BONGO MOVIES, JOHN MAGANGA.


 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salamu za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
Wasanii wa Bongo Movies wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
 
Msanii wa Bongo Movies,  Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movies, marehemu  John Maganga leo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa msanii, John Maganga, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam leo.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba (kulia).
                                                                (Picha na Bashir Nkoromo)

VILIO, SIMANZI VYATAWALA MSIBA WA JOHN STEVE MAGANGA.


Wasanii wa filamu wakiingiza mwili wa Maganga nyumbani kwao Mwananyamala A.
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya jeneza.
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, akiteta jambo  na rais wa wasanii wa filamu.
Padri  Evodius Miku wa Parokia ya Mwananyamala akinyunyiza maji ya baraka kwenye jeneza.
Dada wa marehemu, Janeth (katikati) akilia kwa uchungu.
Baba wa marehemu, Stephano Maganga (kulia), akiwa na uso wa huzuni.
                                                   Waombolezaji wakifuatilia tukio hilo.
ILIKUWA ni simanzi kubwa kwa  wasanii nchini  waliofika kwenye msiba wa msanii wa filamu, John Steve Maganga,  kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.  Maganga aliaga  dunia Jumamosi  iliyopita na maziko yake kufanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo watu wengi walihudhuria.
                                                   NA HARUNI SANCHAWA, GPL

MAKANISA YA KIROHO VITA NZITO.

Stori: Haruni Sanchawa na George Kayala - Chanzo cha habari www.globalpublishers.info
VITA nzito imeyakumba makanisa ya kiroho nchini baada ya wachungaji wao hivi karibuni kurushiana maneno makali hadi wengine kutamka kuwa wenzao wanadanganya waumini ili kujipatia fedha.
 
Aliyeanzisha mtifuano huo ni Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako ambaye alikwenda mbali zaidi na kuwaonya waumini wa Kikrito kujiepusha na watumishi wa Mungu wanaojiita mitume na manabii, akidai kuwa wanafanya utapeli wa mchana.
Kwenye mahubiri yake kupitia kipindi  kilichorushwa hewani na Televisheni za Channel 10 na C2C za jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mzee wa Upako, aliwaambia waumini  kutoka makanisa ya Anglikana, Lutherani, SDA na Roman Katoliki waliojiunga na makanisa ya kiroho kuwa  ni bora wakarudi katika makanisa yao ya awali kuliko kwenda katika makanisa ya wanaojiita mitume na manabii.
 
“Makanisa yetu haya ya kiroho ni hovyo, wameingia matapeli na ninayasema hapa haya kwa kuwa ninayajua, nipo ndani ndiyo maana najua kitu ninachokisema na mtu akitaka tubishane kwa hoja hii, hawezi kunishinda.
“Najua hili ninalozungumza ni jambo zito na ni vita lakini ninaposema haya maneno ni sauti ya Mungu mwenyewe inatoka kupitia kinywa changu. Sitakuwa tayari kama mtumishi wa Mungu kuona watu wakiibiwa halafu nikaendelea kukaa kimya,” alisema Mzee wa Upako.
 
Aliongeza kuwa ni bora aache kazi ya uchungaji anayoifanya, arudi kijijini kwao akawe mkulima kuliko kukaa kimya akishuhudia watu wakiibiwa fedha zao na watu wanaojiita mitume na manabii.
 “Siyo siri, serikali inatambua Kanisa la Romani Katoliki, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kanisa la Anglikana Tanzania,  Kanisa la Mennonite na kidogo kwa sasa Kanisa la SDA.Makanisa yetu tunayoyaongoza ya kiroho nami nikiwamo, serikali haiyatambui na imetokana na watu kujiita mitume na manabii.
Baadhi ya watu wanaojiita mitume na manabi ni Josephat Mwingira wa Kanisa la Huduma ya Efatha, Onesmo Ndegi  wa Living Water, Flora Peter wa Kanisa la Maombezi na Moses Kingu.
WALICHOSEMA WANAOJIITA MITUME
Gazeti hili liliwatafuta watu wanaojita mitume au manabii na walionesha kuna bifu kati yao na Mzee wa Upako kwani walikuwa na haya ya kusema:
Mtume Moses Kingu:
 
“Kila mtu ana  uhuru wa kusema, kauli aliyoitoa Mzee wa Upako huo ndiyo mwisho wa fikra zake, pengine alisema hivyo kwa kulinda watu wake wasimkimbie. Kauli yake hiyo ni ya kujiweka sawa, ukisoma  Agano Jipya unakutana  na ufafanuzi wa mitume na manabii.”
Naye Nabii  Onesmo Ndegi alisema: “Mzee wa Upako anatafuta umaarufu kwa kutumia kauli zake hizo kwani  hata Biblia inatutambua. Angalia Wakorinto1, mlango wa 12  mstari wa 28 unaeleza kazi za manabii na mitume, anayesema mitume na manabii hawapo huyo ni mkorofi.
 
Kwa upande wa Nabii Flora alisema: “Huduma ya maombezi ni ya Mungu na mtumishi wa Mungu wa kweli hapaswi kumsema  mtumishi mwenziye. Mtu wa namna hiyo kinachomsumbua ni wivu wa waumini na utajiri na huwenda huduma yake imeanza kutetereka.
Nabii na Mtume Mwingira hakuweza kupatikana lakini katika kitabu chake  alichokiita Wito Wangu na Kusudio Nililopewa, ameandika kuwa utume wake ni wa kupewa na Mungu.
Mwingira anasema  alikuja kuchukuliwa duniani na malaika na akaenda mbinguni kwa kutumia ngazi.
 
Anaongeza kuwa malaika aliyekuja kumchukua alimpeleka moja kwa moja kwa Yesu ambaye alimkumbatia na akampeleka Jehanamu kuuona moto wa waovu.

Ajali zazidi kuitesa Tanzania Lori lenye namba za usajili T 229 AVP jana lilipata ajali mpakani mwa mkoa wa Njombe na Ruvuma na kujeruhi dereva na msaidizi wake.

                                                         Via songeayetu.blogspot.com
Lori lenye namba za usajili T 229 AVP jana lilipata ajali mpakani mwa mkoa wa Njombe na Ruvuma na kujeruhi dereva na msaidizi wake
Lori hilo lilikuwa limebeba shehena ya mbolea kwenda mkoani Ruvuma

Majeruhi akiwa amebanwa ndani ya gari
Moja kati ya wasamalia akijaribu kumtoa dereva aliyekandamizwa ndani ya gari bila mafanikio. 

Gari aliyopata nayo ajali mpendwa wetu sharo milionea ni hii hapa.

R.I.P BROTHERS! Ni pigo kwa wasanii na Tanzania kwa ujumla

Walalamika wajawazito kutozwa fedha na Vitenge kinamama wajawazito wanapokwenda kujifungua Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Habari na Hillary Shoo, Manyoni.
WANANCHI wa kijiji cha Mwanzi, wameilalamikia Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kutokana na kitendo cha kuwatoza fedha na vitenge kinamama wajawazito wanapokwenda kujifungua.
Wakazi hao walitoa kilio hicho kwenye kikao maalumu kati yao na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii waliotembelea kijiji hicho kujua utekelezaji wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na jinsia.

“Bora na nyie mmekuja ili nasi tuweze kutoa kilio chetu, ni ukweli usiopingika kwamba unapofika hospitali muuguzi anakuambia kama huna hela utaipata, maana hatukuhudumii, we kaa hapo ukisubiri huduma ya bure. Hapa hakuna huduma ya bure,” alisema Zainabu Juma.
Alisema wamekuwa wakitozwa kati ya sh 20,000 na 30,000, ili kuweza kupatiwa huduma ya kujifungua na wakati mwingine wanaambiwa waende na vitenge 20.

“Hivi kweli jamani vitenge 20 vya nini, mimi najua kuwa huduma kwa kinamama wajawazito zinatolewa bure, lakini hapa Manyoni hilo halipo,” alilalamika.
Akijibu malalamiko hayo, Dk. Mapela alisema ni makosa kumtoza mama mjamzito fedha, kwani huduma hizo zinatolewa bure.

Kwa upande wake, muuguzi kutoka Hospitali ya Manyoni, aliwataka kinamama hao kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wahusika, ikibidi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ili wanaofanya mchezo huo wawajibishwe.

Amuua mama yake kwa mateke na ngumi.

MKAZI wa Swaya, jijini Mbeya, Ndele Julius, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, iliyotumwa kwa waandishi wa habari jana, ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 25, mwaka huu, eneo la Swaya.
Taarifa hiyo ilimtaja mwanamke huyo aliyeuawa kuwa ni Sinjembele Julius (62), aliyekuwa mkulima.

“Chanzo cha kifo hicho ni mtuhumiwa kuwa na ugomvi na kijana mwenzake ndipo mama yake alipokwenda kuamulia ugomvi na kugeukwa na mwanaye kisha kuanza kushambuliwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.Ilielezwa kuwa baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikimbia, hivyo Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu au watu wenye taarifa juu ya mahali alipo mtuhumiwa, ili akamatwe au ajisalimishe mwenyewe. Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya

MANENO YA MWISHO YA SHARO MILIONEA KATIKA ACCOUNT YAKE YA TWITTER USIKU WA JANA.

Maskin kumbe kukurupuka na kuhis karogwa ulikua unakifata kifo chako na ona unavyosema hauko poa haukuwa poa kweli ilikua sku yako ya kufa R.I.P Sharo.

Zitto ampa mtihani Prof. Muhongo Ashindwa kujibu hoja, adai si mtu wa kulumbana.

SIKU moja baada ya Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, kuibana serikali akiitaka ifafanue juu ya upotevu wa sh bilioni 86 za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amekwepa kuzungumzia suala hilo.
 
Wakati Waziri Muhongo akikwepa, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Jenerali mstaafu Robert Mboma, nao walishindwa kutoa ufafanuzi.

Katika taarifa yake juzi, Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), akinukuu taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyobaini upotevu wa mabilioni hayo pamoja na mambo mengine alimtaka Waziri Muhogo aeleze hatua alizochukua baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo kuhusu maofisa waandamizi wa wizara waliohusika na wizi huo.
Hata hivyo katika hatua ya kushangaza, Waziri Muhongo, alipotafutwa kwa njia ya simu ili azungumzie juu ya upotevu huo wa mabilioni ya shilingi, alisema hana cha kujibu na kwamba taarifa hizo yeye hajazisoma.

Alipotakiwa kuelezea hatua alizozichukua yeye kama waziri dhidi ya wizi huo, Prof. Muhongo, hakuwa tayari bali alisema yeye sio mtu wa kulumbana na kwamba kama kuna fedha zimeibiwa kuna taratibu za serikali.

“Tuongee mambo ya maendeleo, kuna wengine kulumbana ni kazi yao; sisi wengine taaluma zetu sio hizo,” alisema Prof. Muhongo.
Mapema gazeti hili lilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi, kuzungumzia taarifa hizo bila mafanikio.

Zitto katika taarifa yake mbali na Wizara ya Nishati na Madini pia alimtaka Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma juu ya kiwango cha fedha ambacho Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme wa dharura kati ya Novemba 2011 na Oktoba 2012.
Alipotafutwa, Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kuzungumzia juu ya suala hilo, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alivyotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi pia hakujibu.

Juzi, Zitto alibainisha juu ya kuwapo kwa ripoti zinazoonyesha kuwa kuna kikundi ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia kwenye ununuzi wa mafuta mazito ya mitambo ya IPTL.
Alisema juhudi zilizofanywa na Kamati ya Bunge ya Hezabu za Mashirika ya Umma ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Nishati na Madini, January Makamba, za kutaka uchunguzi juu ya suala hilo ufanywe, hazikuzaa matunda.

Katika kutafuta kiini cha upotevu, kwa mara nyingine, wa mabilioni ya shilingi TANESCO, gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jenerali mstaafu Robert Mboma, bila mafanikio.
Hata hivyo, alipopigiwa Makamu Mwenyekiti wake, Victor Mambalaswa, alisema yuko jimboni na kwamba taarifa hiyo ya CAG kuhusu upotevu wa mabilioni hayo haijafika TANESCO.
“Kama kuna mtu kaiona hiyo taarifa itakuwa serikalini lakini TANESCO bado haijafika,” alisema Mwambalaswa.
Kwa upande wake Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Mnyika, alisema anaungana na Zitto kuwataka viongozi hao wa serikali watoe kauli kwa umma akiwamo CAG na Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).

Alisema iwapo kauli hazitatolewa kwa wakati atatoa nyaraka na majina ya wahusika.
Mnyika alisema alichoeleza CAG kwenye taarifa yake kama ilivyonukuliwa kwenye gazeti la The East African la Novemba 24-30 kuhusu dola milioni 54 (bil. 86) ni sehemu tu ya tuhuma za ufisadi zinazotokana na ukiukwaji wa sheria ikiwemo ya ununuzi katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.Via Tanzania Daima.
“Lakini ukweli kuwa tuhuma za ufisadi, Waziri Muhongo, Waziri Mgimwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Jenerali Mbona wanapaswa kutoa kauli kurejea taarifa ya Zitto ya jana na taarifa yangu ya Novemba 23 mwaka huu,” alisema Mnyika.

Hivi ndivyo mwili wa sharo millionea ulivokuwa baada ya kupata ajali.

Hivi ndivyo mwili wa sharo millionea ulivokuwa  baada ya kupata ajali.Hayupo hayupo hayupooo hayupooo,, ukienda Bongo Move hayupo hayupo ukienda kwa majuto hayupo ukienda kwa muzik hayupo hayupo Pumzika Kwa Aman broo.

                                   TUNAOMBA RADHI KWA PICHA. 

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate